Fahamu:Penzi La Rayvanny Na Fayma Limerudi kwa Kasi.

Ikiwa zimepita wiki kadhaa na kusemekana kuwa msanii RayVanny na mzazi mwenzie Fayma walikuwa katika mgogoro mzito ulisababisha wawili hao kutengana na mwanamke huyo kubadilisha na kufuta picha za mahusiano.Wawili hao waligombana kwa kile kilichodaiwa ni wivu wa mapenzi.

Hata hivyo baada ya siku kadhaa tangu kuachana kwa wawili hao , msanii RayVaanny alianza kuandika kuwa amem-misi mtoto wao wa kiume ambae ameondoka nyumbani na mama yake , hata hivyo bado kuachana kwao kulianza kuthibitika baada ya msanii huyo kuonekana akiwa nje ya nchi lakini akiwa na mwanamke wa kizungu ikisemekana kuwa alikuwa ni mrithi wa fayma, mama wa watotowake.

download latest music    

Lakini kumbe wanaogombana ndio wanaopatana kila siku,ikiwa ni kama siku tatu zimepiata mpaka leo msanii RayVannya aliachia ngoma yake mpya ambayo inajulikana kwa jina la SIRI ambapo katika video hiyo alitumika kama video queen ni mama wa mtoto wake huyo.

Hii ina maanisha kuwa wawili hao hata kama walikuwa na tofauti zao basi zilishakwisha na kuamua kufanya kitu cha pamoja au kuachana kwao ilikuwa ni kuweka kiki ili kuweza kuvuta attention ya watu kwa ajili ya wimbo huo mpya.Akitambulisha wimbo huo katika akaunti yake ya instagram,RayVanny aliandika kuwa

sikukupata kwa bahati mbaya kwanini nikuache kwa makusudi,NAKUPENDA MAMA JAY #SIRI link in my bio

Katika wimbo huo mpya wa Rayvanny ,Fayma ametuma kama video queen na ameonekana kuitendea vizuri video hiyo, huo sio wimbo wa kwanza kwa Fayma kuweka katika nyimbo ya Rayvanny.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.