Fahyma Adai Haoni Sababu Ya Wimbo Wa Rayvanny Kufungiwa

Mpenzi wa staa wa Bongo fleva kutoka katika label ya WCB Rayvanny, Fahyvanny ameibuka na kumkingia kifua Mpenzi Wake kuhusu sakata la BASATA kufungia nyimbo yake ya Mwanza.

Siku chache zilizopita Rayvanny na Diamond waliachia nyimbo yao mpya lakini muda mchache Baada ya kuachiwa BASATA waliifungia kwa madai ya kukiuka maadili ya Kitanzania.

download latest music    

Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Fahyvanny amedai wimbo wa mzazi mwenziye uliofungiwa ni kwa ajili ya kuburudusha vijana na sio watoto kwa hiyo ziwekwe sheria ambazo zitawapa wasanii uhuru wa kubuni vitu vizuri kwa kuwa sio wote wameuelewa wimbo huo kutokana na ubunifu uliotumika.

Nimejisikia vibaya sana kwa sababu ni kazi ya mume wangu halafu ni kazi ambayo naipenda sana, lakini pia wamepoteza pesa nyingi na muda kurekodi halafu wanafungia wimbo kirahisi tu, wanaposema wimbo hauna maadili huwezi jua kila mtu anaposikiliza anakuwa ana mtazamo wake.

Mimi sioni tatizo kwenye huo wimbo kwa sababu umetungwa kwa ubunifu wa hali ya juu mbona nchi za wenzetu hawana haya mambo jamani tena kama Nigeria wanaandika kabisa kuwa muvi hii ni kwa ajili ya watu walio juu ya miaka kumi na nane”.

Baada ya wimbo huo kupigwa stop kupigwa BASATA iliwatoza WCB faini ya milioni 9 na kukataza kabisa wimbo huo kupigwa sehemu yoyote nchini na kuwakataza wasanii kuperfome wimbo huo stejini.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.