Faiza Ally aachia picha za mtoto wake, Lil Junior

Muigizaji wa Bongo muvi ambaye pia ni mwanabiashara , Faiza Ally, alijifungua mtoto wa kiume na amempa jina la Lil Junior.

Faiza Ally

Mrembo huyo pia hivi Leo amewachia picha kadhaa kumuonesha mtoto wake ambaye anaaminika kuwa muindi au mzungu. Kupitia mtandao wake wa Instagram aliandika kusema;

download latest music    

“Asanteni sana ndugu zangu Watanzania nimeishiwa na maneno kwa mapenzi yenu. Najiona kila kona kwenye kurasa mbalimbali za marafiki, umbea, habari yaani najihisi kupendwa. Na nimezidi kutambua kuwa uwepo wangu upo, naomba niwaambie nawapenda sana, natambua uwepo wenu wote, natamani ningejibu kila comment , nipite kila kurasa, nijibu msg zote DM na WhatsApp ndiyo usipime yote hayo ni mapenzi, najisikia baraka kwa kweli, furaha yangu inazidi mara dufu ALHAMDULILLAH. Nawatakia kila la kheri na baraka tele kwenu, wanaotafuta watoto Mwenyezi Mungu awajaalie kila la kheri mpate, na waliopata INSHAALLAH, Mwenyezi Mungu awatunzie wawe watoto wenye baraka kwenu AMEN YARAB. Nawapenda Watanzania, naipenda Tanzania, Mungu tubariki sisi na vizazi vyetu AMEN.”

Tazama picha hiyo hapa;

About this writer:

Pauline Syombua

Content Developer IG: Kermbua