Faiza Ally Adai Sugu Bado Ana Mapenzi na Yeye

Muigizaji wa Bongo movie na mjasiriamali maarufu Faiza Ally amefunguka na kudai mzazi mwenzake Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ bado anampenda.

Faiza amefunguka hayo baada ya sakata lao la juzi ambapo Faiza alimtolea povu Sugu Kwenye mitandao ya kijamii na kumtaka amuheshimu baada ya Sugu kumtuma Mke wake kufanya shopping ya Faiza badala ya kumpa pesa.

download latest music    

Faiza amemwaga povu hilo Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers kwenye ‘sherehe ya 40’ ya Zamaradi Mketema na kufunguka mengi ikiwemo utayari wa kurudiana na Sugu iwapo atarudi walee mtoto wao.

Nadhani Sugu bado ananipenda ndiyo maana hatimizi vizuri wajibu wake wa malezi na matumizi kwa mtoto wake Sasha. Huenda anafurahi mimi ninavyokuwa ninamsema na mimi siwezi kuchoka kumsema mpaka pale atakapoweza kutimiza majukumu yake ipasavyo.

Kama huhitaji kuwa na ishu na mtu basi unaweza kufanya mambo kwenye right way (njia sahihi), lakini ukiona mtu anakutafutia vitu vya kukuumiza ujue bado uko kwenye moyo wake, aweke pesa ya matumizi ya mtoto kwenye akaunti kila mwezi, atimize majukumu yake then ataona kama mimi nitaendelea kumfutalia”.

Faiza na Sugu wamekuwa kwenye mgogoro wa muda mrefu wa kifamilia hasa kuhusu suala la malezi ya mtoto wao Sasha.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.