Faiza Ally amchana Hamisa Mobetto

Faisal Ally ambaye anajulikana sana kwa sababu ya movie zake za Bongo na pia mitindo yake ya kimavazi hivi karibuni alifunguka kuongelelea ujauzito wa Hamisa Mobetto ambaye ni video vixen na model kutoka bongo.

download latest music    

Hata hivyo hii ndio mara ya kwanza Faiza Ally kutoa maoni kuhusu mrembo huyu tangu isemekane kuwa anamtarajia mtoto wa Diamond Platnumz ambaye ni mume wa Zari Hassan.

Akizungumza na 3 Tamu, Faiza alisema kuwa, yeye Kama mwanamke hajafurahishwa na maneno yale ikiwa ni kweli kuwa Hamisa Mobetto ana ujauzito unaodaiwa ni wa msanii wa CEO wa Wasafi Records. Ally alisema,

Unajua wasichana wengi hawajithamini wanafanya vitu bila kufikiria, kama huyo Hamisa nasikia ana ujauzito wa huyo msanii (jina kapuni) na kama ni kweli mimba ni ya huyo mtu, kakosea sana, napenda kuongea kitu kinachonigusa kwenye nafsi yangu akichukia atajijua.

Hata hivyo Diamond aliweka wazi hivi karibuni kuwa yeye na Hamisa Mobetto hawamtarajii mtoto pamoja na kuwa uhusiano was ni wa kibiashara tu.

About this writer:

Pauline Syombua

Content Developer IG: Kermbua