Faiza Ally Amtolea Povu Zito Sugu

Muigizaji wa Bongo movie na mjasiriamali maarufu Faiza Ally amemjia juu mzazi mwenzake ambaye ni Mbunge wa Mbeya Mjini na msanii mkongwe wa Bongo fleva Sugu.

Sugu na Faiza wamezaa mtoto mmoja anayeitwa Sasha lakini wamekuwa kwenye mgogoro wa kifamilia kwa muda mrefu sana ambapo Faiza amekuwa akidai kuwa Sugu anagoma kumlea mtoto.

download latest music    

Wawili hao walionekana kumaliza tofauti zao mwezi uliopita baada ya Sugu kutoka jela ambapo Faiza aliandika Kwenye mitandao ya kijamii kuwa yeye na Sugu wamemaliza tofauti zao.

Lakini Faiza amemtolea povu Tena Sugu siku ya leo ambapo kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika:

Natuma barua kwako kwa sababu ndio sehemu pekee ya kukufikishia ujumbe na ukaupata! Ni hivi tangu tumeachana Sasha akiwa na mwaka mmoja na miezi sita mpaka leo hijatafuta njia sahihi na yenye heshima mimi sio wa kufanyiwa shopping na happy eti nikachukue Mlimani hiyo ni dharau sana Baba kama ulikosa muda ungetuma hela! Lazima uweke heshima kwa Baby mama wako na mwanao! Sasa ni hivi siwezi kwenda kuchukua sukari na maziwa Mlimani ni dharau”.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.