Faiza Ally- Ipo Siku Watu Wataelewa Ndoto Zangu

Muigizaji wa Bongo movie na mzazi mwenzake na Mbunge wa Mbeya mjini na msanii Joseph Mbilinyi ‘Sugu’, Faiza Ally ameibuka na kudai ipo siku watu wataelewa tu ndoto zake.

Faiza Ally amefunguka kuwa watu wengi wanaweza wasimuelewe kwa jinsi anavyopigana na maisha ili tu kutimiza ndoto yake ila ipo siku wataelewa.

download latest music    

Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers Faiza alisema anakesha China, kubeba mizigo ya watu waliyomuagiza vitu kwa sababu anatafuta pesa na nia yake kubwa ni kuwa tajiri tena kwa kutafuta kwa jasho.

Naona watu hawanielewi mimi ni kukesha na kubeba mizigo ya watu walioaniagiza ni kwa sababu nausaka utajiri tena siyo hela ya haramu ni ya jasho langu na ninataka kuonyesha watu inawezekana na ipo siku watanisimulia tu”.

Mpaka hivi sasa Faiza amekuwa nchini China kwa muda wa wiki kadhaa na amekuwa akionekana akiwa ananunua bidhaa  mbali mbali kwa ajili ya kufanyia biashara anazoagizwa na wateja Wake.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.