Faiza Ally na Mke wa Mbunge Sugu Kwenye Bifu Kali

Faiza Ally ambaye ni muigizaji wa Bongo movie na mama watoto wa Mbunge wa Mbeya mjini Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ amezidi kutibuana na mpenzi wa Sugu anayejulikana kama Happiness Msonga.

Faiza ambaye hajawahi kuficha hisia zake kuwa bado anampenda Sugu licha ya wawili hao kuachana, Sugu ameweka wazi uhusiano wake na mpenzi wake happiness ambaye amekuwa kimya kwa muda mrefu akivumilia maneno yote ya kejeli kutoka kwa Faiza.

download latest music    

Kupitia ukurasa wake wa instagram Faiza alimrushia maneno na kudai kuwa Happiness anamtumia watu wamtukane kwenye mitandao ya kijamii na anafungukua kurasa feki ili kumtukana Faiza na pia amedai kuwa Sugu hawezi kumuoa Happiness kwa sababu ameshaolewa ndoa ya kanisani na mwanaume mwingine anayejulikana kama Minja.

Unafungua account feki unanitukana si unitukane kwenye account yako tupambane sasa kwani uongo? We sio mke wa mtu? Kwa umaarufu gani uwe na fan page zaidi ya sita Na zingine special kwa ajili ya kunitusi? Unajifanya innocent mbele za watu kumbe joka jeusi Mungu anakuona na usaliti kwenye ndoa …pole kaka ninja muwe mnaangaliaga Zaidi mavazi ya kuna vigezo vingi kabla ya kuoa Sio muonekano”.

Pia Faiza hakuishia hapo aliwajia juu mashabiki wote wa Happiness na Sugu waliokuwa wanadai kuwa Happiness ndio wife material yaani ndo mke wa kuoa siyo yeye.

Acha nijibu miye siwezi kunyamaza nisije nikaumwa presha …huyo happy mnaomsifia ni wife material kwa umaterial gani? Au kwasababu Ana ndoa ya kanisani na kamkimbia mumewe kwaajili ya mbunge? au hamjui kwa mini ndoa haifingwi?  na huyo mbunge atafanyeje naye anapenda mteremko wanawake wazuri wanataka matunzo? wamekutana woye mabandidu bora hata baba Sasha ana mvuto kidogo ila huyo mwanamke hamna kitu”.

Pia Faiza alisisitiza kuwa kati yake na Happy yeye ndio mrembo na Happy ni mbaya, sababu ya ugomvi wao Faiza anamzuia mtoto wa Sugu kumuona baba yake.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.