Faiza Amshauri Diamond Kuachana Na Zari Ili Apate Muda Wa Kula Ujana.

Baada ya kuenea kwa tetesi kuwa msanii mkubwa wa muziki bongo na mzazi mwenzie Zari The Bossy wanawezekana kuwa katika mgogoro mzito kutokana na tetesi zinazoenea kuwa msanii huyo kwa sasa anatoka kimapenzi na video queen Tunda , Faiza Ally amemshauri Diamond kuachana na stress za kuachana na mzazi mwenzie na kama anataka kumuacha amuache tu kwa sababu yeye bado ni kijana sana bado anahitaji kula ujana.

Faiza anamwambia Diamond kuwa aache kujibebesha mizigo ya kuwa na familia wakati yeye bado ni kijana na anahitaji kutumia ujana wake vizuri kabla umri wake wa kujibebesha majukumu haujafika.

download latest music    

Diamond ni kijana mdogo sana anahitaji kuhave funny na watoto wenzie sio wadada watu wazima, lazima tuangalie watu wa kutembea nao.go baba enjoy the World have funny ndio useto down.jiachie uwe huru ikibidi usiwe na mahusiano kabisa.bado ujaona Dunia hata robo, wewe ni star ela ipo . there is a lot to see nasema with a clean hate no hate  kwa zari na kwa yoyote.

Sio kwa mara ya kwanza Faiza amekuwa akitoa ushauri kwa Diamond kutokana na matatizo yanayomkumba hasa kwa mambo ya mahusiano na jinsi wanawake alionao katika mahusiano wanavyokuwa wanampelekesha.

Itakuwa ni mara ya pili sasa Diamond na Zari wanaingia katika mpasuko wa kimapenzi baada ya kuwa natetesi nyingi zinazokuwa zikisambaa kwamba mwanaume huyo yupo katika mahusiano ya kimapenzi na watu wengine.Mara ya kwanza ilikuwa Hamisa Mobeto na sasa ni mrembo Tunda.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.