Faiza: Ina Maana Watanzania Wote Hamkuwaona Mpaka Mkampe Dili Zari

Muigizaji wa Bongo movie na mfanyabiashara maarufu Faiza Ally amerudi tena Kwenye headlines baada ya kutoa povu zito Baada ya Zari kutangaza kama balozi mkuu wa bidhaa za Softcare.

Siku ya jana Zari pamoja na kampuni ya Softcare walifanya mkutano na waandishi wa Habari ambapo walimtangaza Zari kama Balozi wa kuuza Bidhaa hizo ambazo ni pampas za watoto.

download latest music    

Lakini dili hilo lilizua minong’ono kutoka kwa watu hasa kwa sababu kampuni ni ya Tanzania lakini Zari ni Mganda anayeishi nchini South Africa kwaiyo inakuwaje waache mastaa wote wa hapa Tanzania waende Uganda.

Faiza alitoa povu zito juu ya hilo na kuihoji kampuni hiyo kwa nini imewaacha wanawake wengine wengi ambao ni mastaa hapa Tanzania ambao nao wengeweza kufanya kazi hiyo na kumchukua mtu ambaye hata sio Mtanzania.

Kupitia ukurasa wake wa instagram Faiza alitoa povu hili:

Hii sio mara ya kwanza kwa Watanzania kulalamika baada ya Zari kupewa Dili la kutangaza bidhaa za Tanzania alishawahi kuwa balozi wa Danube na Vodacom.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.