Faiza- Nikipata Ukimwi Nitajitangaza Hadharani

Muigizaji wa Bongo movie na mzazi mwenzake na Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi ‘Sugu’, Faiza Ally amefunguka na kuweka wazi kusababisha endapo siku akijigundua kuwa ni muathirika basi hatajificha bali atajitangaza hadharani.

Faiza amefunguka kuwa endapo itatokea bahati mbaya akakwaa ugonjwa wa Ukimwi a.k.a ngoma, kamwe hatajificha au kujiona tofauti, bali atajitangaza hadharani na kuwapa watu moyo kuwa wanaweza kuishi miaka mingi zaidi.

download latest music    

Katika mahojiano yake na Gazeti la Ijumaa, Faiza ambaye ni mama wa watoto wawili alisema anawashangaa wenye tatizo hilo ambao hujificha na hata wengine kuambukiza wengine, lakini kwa upande wake ataweka hadharani ili kuwapa elimu wengine na kuzuia maambukizi mapya.

Kama mimi ningekuwa na Ukimwi, ningejitangaza hadharani bila woga wowote wala aibu na tena nitasaidia watu wengine wajiepushe na maambuzi mapya“.

Wiki iliyopita Faiza alizua gumzo kwenye Mitandao ya kijamii Baada ya kuposti video iliyomuonyesha akiwa anapima ugonjwa wa Ukimwi na kuanika majibu yake yaliyoonyesha hana maambukizi ya gonjwa hilo.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.