Ferooz Atangaza Kujipanga Upya.
Msanii ferooz amekiri kuwa katika game la muziki kwa sasa kuna utofauti mkubwa sio kama ilivyokuwa zamani kutokana na ukweli kuwa kumekuwa na wasanii wengi chipukizi ambao wanafanya vizuri sana katika muziki.
Ferooz anasema kuwa kwa sasa anataka kurudi katika game lakini kitu cha kwanza anataka kukifanya ni kujipanga na kuangalia ni jinsi gani anaweza kuwa sawa na wale waliopo katika game kwa sasa kwa kuisoma ramani ya muziki wa sasa na sio kurudi kama walivyozoea hapo awali,
Ferooz ambae aliwahi kutamba sana miaka ya nyuma hasa kwa wimbo wake wa starehe anasema kuwa muziki ni kama maisha kuna sehemu utapanda sana na kuna sehemu unaweza kushuka kabisa lakini swala la muhimu ni kuangalia ulipojikwaa na kurekebisha tena.
muziki uko kama maisha ya kawaida kuna kupanda na kushuka, ila kwa sasa niko napmabana ili niweze kupanda tena .
Ferooz anasema kuwa ana nyimbo mbili ambazo ataziachia mfululizo hivi karibuni na anaomba mashabiki wakae mkao wa burudani zaidi.