Feza Kessy Akiri Kumtongoza Cyrill Kamikaze.

Msanii wa kike wa muziki wa kizazi kipya nchini , Feza Kessy amefunguka na kuongelea ukweli juu ya kudai kuwa alishawahi kufanya kitendo abacho huwa ni kigumu sana kwa wanawake wengi kuthubutu kufanya kutokana na uoga na aibu kwa watu wanaowafata na uwafanyia kitendo hicho.

Feza Kessy alisema kuwa alishawahi kumtongoza mwanaume aliyewahi kuwa na hisia nae baada ya kuona kuwa hawezi kuvumilia na kukaa kimya.

download latest music    

Feza Kessy anasema kuwa baada ya kukaa kwa muda mrefu bila kuwa na mahusiano baada ya kuachana na aliyekuwa mpenzi wake alijikuta akiwa na hisia za kimapenzi na mwanamuziki mwenzie Cyril Kamikaze  kwa muda mrefu tangu alipokuwa katika mahusiano yake ya awali na kuamua kumwambia ukweli ili ajue.

Hata hivyo Feza Kesy anahadithia na kusema kuwa pamoja na kwamba alipata ujasiri na kumtongoza kamikaze lakini Kamikaze alimtolea nje na alipoona kuwa bado anamsumbua  na hataki kuamini kuwa yupo katika mahusiano   Kamikaze aliamua kumtolea uvivu na kumwambia mwenzi wake ambae nae pia hakusita  kumuomba aachane na bwana wake.

Kwakweli nilikuwa ninam-like sana sana,lakini yeye alikuwa anan-like kidogo kidogo na kwa kipindi kile alitakiwa kuja na kunibembeleza plus  kuumizwa nikaona bora nitangaze nia kwa kweli na yeye akawa ananiambia ooh sijui nina mtu,sasa na mimi nikawa siamuamini nikajua kuwa ananipima lakini baadae na mtu wake alikuja akanifata inbox kuniomba niachane na mtu wake.

Hata hivyo baada ya Cyril kumkata Feza Kessy bado tu wawili hao waliendelea kuwa  marafiki na wamekuwa wakiwasiliana vizuri bila shida yoyote.

Hapo kipindi cha nyuma wawili hao walikuwa wakionekana pamoja katika baadhi ya sehemu na kuhisiwa kuwa ni wapenzi ingawa kwa upande wao wenyewe walikataa kuwa na mahusiano, hatimaye Feza mwenyewe ameamua kuthibitisha hilo.

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.