Feza Kessy Ataja Sifa za Mwanaume Anayemtaka

Msanii wa Muziki Bongo fleva Feza Kessy amefunguka na kuweka wazi sifa anaziziangalia kwa mwanaume ambaye anataka kuwa kwenye mahusiano naye ya kimapenzi.

Feza amekuwa kwenye headlines siku chache zilizopita hasa kwa sababu ya skendo yake ambayo imekuwa ikimuandama kwa muda mrefu kuwa ni msagaji tetesi ambazo amezikataa.

download latest music    

Kwenye mahojiano na kipindi cha Refresh cha Wasafi Tv, Feza amesema kutoka moyoni yeye hapendi mwanaume hawezi kujituma na wala hawezi kuwa kwenye mahusiano na mwanaume ambaye hajui majukumu yake;

Kwanza napenda sana mwanaume ambaye anamuogopa sana Mungu na ambaye anapambana sana kumjua Mungu kabla yangu mimi lakini namba mbili napenda mwanaume mwanaume yaani sio wanaume wa Dar.

Napenda mwanaume ambaye amekaa kiume sio wale wanaume wa Dar mabrazameni yaani nataka mwanaume ambaye anafanya kazi za kiume na ambaye haogopi kuchafuka na ambaye atakuwa pale kwa ajili ya kunilinda”.

Lakini pia Feza amedai mwanaume anayemtaka sio lazima awe na pesa nyingi sana ila awe tayari kufanya kazi kwa ajili ya kuiangalia familia yake.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.