Fid Q aeleza uwezekano wa kutoa remix ya pili ya ngoma yake ya utata ‘Fresh’

‘Fresh’ remix imezua utata kwani Diamond alijibu tuhuma kuwa yeye ndo baba wa mtoto wa Hamisa Mobeto kwenye verse yake kwa hio wimbo ‘Fresh’. Diamond pia alimchimba Alikiba kwa wimbo huo huo.

Sasa kuna uwezekano kuwa remix ya pili ya ‘Fresh’ kutolewa (ngoma ya ‘Fresh’ original ilitoka August 13 ). Fid Q alikua atoe remix ya ‘Fresh’ na msanii ZaiiD lakini mwishowe aliamua kuwashirikisha Diamond na Rayvanny.

download latest music    

Fid Q hata hivyo aliambia XXL ya Clouds FM kuwa hajamsahau ZaiiD kwani kuna mpango wa kutoa remix ya pili ya ‘Fresh’ ambayo atamshirikisha ZaiiD.

“Nilipotoa Fresh ZaiiD aliniambia please kama utatoa remix na mimi niwepo, kwa hiyo ilipokuja kutokea hii nyingine siyo kama nimemsahau, hapana kuna mipango mingine inafanyika, huenda kukawa na remix nyingine lakini alinishtua kwamba nataka kuwepo na ni moja ya marapa ambao napenda sana michano yao na bila shaka hato-disappoint,” Fid Q alisema.

About this writer:

Martin Oduor

Ultimate keyboard ninja dedicated to bringing you the juiciest stories on blogosphere