Flaviana Matata Amkingia Kifua Jokate Kwa Wanaomponda Kuwa DC

Mlimbwende na Model wa kimataifa Flaviana matata amefunguka na kumkingia kifua Mrembo Jokate Mwegelo baada ya kupondwa sana baada ya kutangazwa Mkuu wa wilaya siku chache zilizopita.

Siku chache zilizopita Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli alimteua Jokate Mwegelo kuwa mkuu wa wilaya ya Kisarawe.

download latest music    

Taarifa hiyo ilipokelewa kwa hisia tofauti tofauti huku wapo waliofurahishwa na taarifa hiyo na kuona Jokate anastahili nafasi hiyo Lakini pia wapo walioona Jokate hastahili kupewa nafasi ya kuongoza wilaya.

Baada ya Mkanganyiko huo mashabiki mbali mbali walianza kuweka mambo ambayo yalikuwa negative huku wakimtupia madongo na asilimia kubwa waliokuwa wanafanya hivyo walionekana kuwa ni wanawake.

Flaviana Matata alishindwa kuvumilia na kumtetea Jokate ambapo kupitia ukurasa wake wa Twitter Flaviana aliwataka wanawake wapendane na wampe sapoti Jokate kwani amepata nafasi ya kusaidia wanawake wengine:

Wanawake hatupendani very sad. Not sure hii itabadilika lini we need to support her na kukumbuka anatuwakilisha wanawake wote”.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.