G.Nako Atabiri Yeye Na Vanessa Mdee Watafika Mbali Zaidi na ‘Wet’

Mwanamuziki wa Bongo fleva anayefanya miondoko ya kurap kutoka kundi la Weusi G Nako ametabiri ngoma yake na Vanessa Mdee inayoitwa Wet kufanya vizuri.

Ngoma ya Wet iliyoimbwa na Vanessa Mdee kumshirikisha G Nako inayopatikana kwenye albamu ya vanessa imeendelea kufanya vizuri na kushika chati mbali mbali nchini.

download latest music    

G Nako amefunguka Kwenye mahojiano na Jembe Fm na kudai kuwa tangua wanatoa wimbo huo walikuwa wameshautabiria makubwa sana kwani walijua ni ngoma kali.

Ni wimbo nzuri toka tulivyoureekodi, wakati albamu bado inaendelea kutengenezwa ilionyesha ni moja ya nyimbo zitakuja kufanya vizuri kwenye albamu.

So nafikiri mafanikio bado yataendelea kuwa makubwa na tunasubiri mafanikio mengine makubwa zaidi na mimi bado nashukuru kwa watu wote ambao wanaendelea ku-support”.

Video ya wimbo wa Wet unaendelea kusimbua kwa sababu ya ubunifu uliotumika Lakini pia umefanywa nchini Tanzania na producer Mtanzania tofauti na trend ya wasanii wengi siku hizi kupenda kushoot video zao nchi za nje kama South Africa na kwingineko.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.