G-Nako Atetea Uamuzi Wake Wa Kutoa Nyingi

Msanii wa muziki wa Bongo fleva anayefanya miondoko ya kurap kutoka katika kundi la Weusi George Sixtus Mdemu maarufu kama G-Nako ametetea uamuzi wake wa kutoa nyimbo mfululizo.

G-Nako amepingana na  madai ya baadhi ya mashabiki zake ambao wamekuwa wakidai mtindo wake wa kutoa nyimbo mpya mara kwa mara kutapelekea kuua  muziki wake.

download latest music    

Malalamiko ya mashabiki wa G Nako kwamba anaua muziki wake, yaliibuka baada ya kutoa Wimbo wa Nyatu Nyatu na kutangaza kuachia wimbo mwingine ndani ya siku chache na Bill Nas, na mashabiki kudai hawapi nafasi mashabiki wa kazi zake kufurahia ngoma bali anawalimbikizia.

Kwenye mahojiano na Global Publishers, G-Nako amefunguka:

Wimbo ukishafika mtaani umefika. Hata ukitoa nyimbo kumi mfululizo mashabiki wana uwezo wa kusikiliza zote.

Zaidi ni fursa kwako kama msanii kwani unaweza kuandaa hata shoo ya peke yako bila kutegemea kuwa na kundi lingine la wasanii”.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.