Gigy Money Adai Anamuacha Mtoto Wake Ili Kusaka Pesa

Video vixen na msanii wa muziki wa Bongo fleva Gift Stanford maarufu kama Gigy Money amekiri kuwa anamuacha mtoto wake nyumbani mara nyingi lakini amesisitiza ni katika harakati za kusaka pesa.

Gigy Money amekuwa akikosolewa sana kutokana na kuonekana akiwa katika kumbi mbali mbali za starehe wakati mtoto wake akiwa na wiki kadhaa tangu azaliwe.

download latest music    

Gigy amefunguka na kujitetea kuwa sababu pekee ambayo inamfanya asafiri na kumuacha mtoto wake nyumbani ni kusaka pesa kwa ajili ya malezi ya mtoto wake.

Kwenye mahojiano na Kipindi cha XXL cha  Clouds Fm amesema ni vigumu yeye kulala nyumbani wakati hana fedha:

Nilienda Nairobi nikakaa mwezi mzima na nilimuacha mtoto na mama yangu, hakuna mtu anaweza kuacha dola 4,000 (sawa Tsh. Milioni 9) kirahisi“.

Gigy Money amesisitiza kuwa ingawa anapenda kukaa nyumbani na mtoto wake Myra lakini amesema hawezi kufanya hivyo kwani Familia yake inamtegemea.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.