Gigy Money Adaiwa Kushushiwa Kipigo Kizito na Dudubaya

Msanii wa Bongo fleva Gift Stanford maarufu kama Gigy Money anadaiwa kutembezewa kipigo cha haja  na msanii mwenzake mkongwe Godfrey Tumaini maarufu kama Dudubaya.

Global Publishers wanaripoti kuwa Tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia Jumapili iliyopita jijini Mwanza ambapo inaelezwa ugomvi ulianza kama utani wawili hao wakiwa nyuma ya jukwaa wakati Tamasha la Wasafi Festival likiendelea.

download latest music    

Shuhuda wa tukio hilo alidai Gigy ambaye mara nyingi ameonekana akiwa karibu na Dudu Baya alikuwa akiongea sana na kutaja mambo ambayo ni matusi mbele za watu huku Dudu Baya naye akiwa na mwanaye.Wakati Gigy akiendelea kumwaga maneno ya chumbani akijihusisha na Dudu Baya, msanii huyo mwenye asili ya utata alikuwa kimya kwa aibu akiwa na binti yake, Maria.

Kukaa kimya kwa Dudu Baya hakukusaidia kitu kwani Gigy aliendelea kutoa maneno makali lakini yalipozidi mwanamuziki huyo aliwaomba waungwana wakamtulize mwanamama huyo.

Yaani maneno ya Gigy yalikuwa yanamfadhaisha sana Dudu Baya na mwanaye  ambapo licha ya kumtaka aache hakusikia, aliendelea tu“.

Kutokana na kuendelea kutoa maneno machafu Dudu Baya alimvaa Gigy na kumshushia kipigo cha ambapo aliokolewa na mabaunsa waliokuwa karibu. Katika varangati hilo Gigy aliangua kilio kutokana na maumivu huku akilalama kupoteza simu yake ya kisasa.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Risasi Mchanganyiko Dudu Baya ili kueleza sababu za kumshushia kipigo Gigy na kufunguka;

Huyu Gigy hana akili, nilishamwambia muda mrefu kwamba sitaki utani wake yeye hanielewi, yule ni mwanamke wa ajabu sana”.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.