Gigy Money Adhibitisha kupata Mtoto Mwakani

Mwanadada asiyeisha vituko kila siku katika mitandao ya kujamii amba pia ni msanii wa muziki anaefanya vizuri kabisa na wimbo wake wa papa amethibitisha kuwa mwakani (mwaka 2018) ni mwaka wake anaotarajia kupata mtoto wake wa kwanza yeye na mpenzi wake.

Akiongea na kituo cha televisheni cha Efm, Gigy Money amesema kuwa mashabiki wake wamtegemee yeye na mpenzi wake kupata mtoto mwakani maana ndivyo walivyopanga.”wategemee tu mwakani nitakuwa na mtoto mungu akinisaidia, yaani hiyo ni lazima kabisa”  amesema Gigy Money

download latest music    

Mwanadada huyo amesema kuwa ulazima huo unakuja pale ambapo yeye na mpenzi wake ambae amekaaa nae zaidi ya miaka  mitatu hivyo ni vizuri kwa sasa kama atampa zawadi ya mtoto,Ingwa hakutaka kumtaja mpenzi wake kwa uwazi zaidi.

baadhi ya mashabiki wamekuwa na hamu pia ya kutaka kujua mwanaume ambae Gigy Money ana mpango wa kuzaa nae kutokaa na scandal nyingi ambazo Gigy Money amezipitia kuhusu wanaume inakuwa ngumu kwa baadahi kuamini kuwa amekuwa na mahusiano ya mapenzi ya kudumu na mwanaume mmoja kwa zaidi ya miaka mitatu huku katika mitandao amekuwa akiuonekana kufanyabaadhi ya vitu visivyoeleweka.

Imekuwa tofauti kwa Gigy Money na wasanii wengi wa kike Tanzania na karibia maeneo mengi Duniani ambao wansadikika kuwa wanogopa kuingia katika swala la uzazi na kubeba mimba wakisema kuwa wanapoteza muda mwingi katika malezi ya ujauzito na mtoto, lakini pia wanakuwa wanapoteza ile shape ya miili yao kwaio inakuwa inaharibu kazi zao za sanaa.

Kwa Tanzania kumekuwa na baadhi ya wasnii ambao wamejitahidi na kuamua kuingia katika majukumu ya kifamilaia huku pia wakifaya vizuri katika kazi za sana mfano ni Linah Sanga, Feza Kessy,Dayna Nyange pia.

Gigy Money ni mwanaddaa asiyeisha vituko kila kukicha ingawa amekuwa akijitahidi katika kazi zake za muziki ambapo kwa sasa anafanya vizuri na kibao chake cha Papa.Amekuwa akiingia katika bifu na mashabiki zake maranyingi na hata musa mwingine  na wasanii wenzie

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.