Gigy Money Ajutia Kuanika Listi Ya Wanaume Aliotembea Nao

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Gift Stanford maarufu kama Gigy Money amefunguka na kuelezea majuto yake kuhusiana na uamuzi wake wa kutaja orodha ya wanaume aliowahi kubanjuka nao.

Siku za nyuma Gigy Money aliwahi kutengeneza headlines baada ya kutaja listi nzima ya wanaume aliowahi kuwa na Mahusiano nao ambapo ndani yake kulikuwa na wasanii kadhaa.

download latest music    

Kwenye mahojiano na Kipindi cha Kikaangoni cha East Africa Tv, Gigy Money amekiri anajutia kutaja orodha hiyo ya wanaume kwani mpaka leo kuna wanaume wanaogopa kumtongoza kwa kuogopa kuanikwa.

Kuwataja wanaume nilipitaga nao najutiaga sana, inafanya kuna muda nikose vitu vya maana kwa kuogopa kuwa nitaropoka. Kumbe ule ni utoto na ni foolish age kila mtu lazima apitie hata uikimbie ni bora uipitie ukubwani usiirudie. Kwahiyo najutia kuwataja wanaume niliowahi kutembea nao ila sijutii kupitia ile hatua“.

Listi ya wanaume wa Gigy Money ilijumuisha mastaa wa muziki wa Bongo Fleva na watangazaji wa Redio na Tv.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.