Gigy Money Alia Kutembezewa Kichapo na Baba Mtoto Wake Wakati Mjamzito

Msanii wa Bongo fleva Gigy Money amefunguka mazito sana yanayomsibu kwa hivi sasa ambapo amedai kuwa baba mtoto wake mtarajiwa ambaye pia ni mpenzi wake wa muda mrefu anayejulikana kama Mo j ana tabia ya kumpiga na amefikia hatua ya kumpiga hivi karibuni akiwa mjamzito.

Gigy Money alitangaza ujauzito wake hivi karibuni baada ya kuuweka Siri kwa muda wa miezi saba huku akiweka wazi kuwa baba wa mtoto huyo ni mpenzi wake ambaye pia ni mtangazaji wa Choice Fm, Mo j.

download latest music    

Siku ya jana kupitia ukurasa wake wa Instagram Gigy Money amlimtupia tuhuma nzito mpenzi wake kwa kudai anamtesa wakati yu mjamzito ambapo amedai kuwa ana tabia ya kumpiga na hata kutembea na wanawake wengine, kupitia ukurasa wake wa Instagram alifunguka yafuatayo;

Kusema ukweli leo nina stress sana ndio maana nimeona bora niseme  kwani ninachokiamini sio peke yangu ninayeyapitia haya katika makosa ambayo naamini nimeyafanya ni kupenda ingawa najua kupenda sio dhambi nimepitia mengi sana kwenye mapenzi hadi kufikia hatua ya kupingua mwili, baadhi ya watu walio karibu na mimi wanaweza wakawa wanajua baadhi ya mateso na utumwa wa mapenzi niliowahi kupitia, mara nyingi unaweza ukatokea kumpenda mwanaume mwenye uwezo wa kawaida ukiamini mapenzi sio pesa lakini wanaume wa Bongo jeuri unabeba mimba dharau atakufanyia mwanamke wake wa nje atakuonyesha kiukweli inauma ndio lakini naamini ni hatua za maisha na ni ukuaji naamini nimedondoka hatua moja lakini nitainuka hatua nane. Tanzania ni nchi inayoongoza kwa kuwa na single mothers sio baba wote wamekufa wengi wetu tunwakimbiza watoto wetu mbali na maisha ya mateso tuliowahi kiyapitia kwa baba zetu ukiona naandika haya yote ujue mambo yamezidi kuwa mabaya”.

Lakini pia Gigy Money amefunguka na kuandika “Nachukia mwanaume anayepiga mwanamke mjamzito, nachukia mwanaume mnyanyasaji na sio kila mwanaume anafaa kuitwa mume”. Lakini Gigy amemfungukia mmoja wa shabiki zake na kusema ni kawaida ya Mo j kumpiga zamani lakini sahivi ameshindwa kuvumilia kwa sababu ni mjamzito.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.