Gigy Money amchana Wema Sepetu kwa Kumuita Fake woman

Hakuna anayejua kilichotokea katikati ya Gigy Money na Wema Sepetu lakini kuna fununu kuwa wawili hawa hawapatani hata kidogo. Hapo mbeleni wengi walijua kuwa Gigy Money anatani kuwa kama Wema Sepetu lakini kwa sasa mambo yamebadilika.

download latest music    

Model huyu wa video za Bongo hivi karibuni alifunguka kudai kuwa Wema Sepetu ni mtu fake na anataka kuwajulisha watu ambao bado hawajapata nafasi ya kumuona live. Akizungumza na Bongo 5 Gigy Money alisema,

“Wema ni mtu ambaye she is fake, Yaah! She is fake. Ukimuona WQema hivi live na ukimuona mtandaoni unaweza ukavurugwa, watu wengi ambao hawajawahi kumuona Wema hivi live wanachanganyikiwa, sio kama mimi sasa hivi. Mimi nilikuwa navurugwa magazeti kila siku nikiensda shule napitia Wema kafanya nini? Sasa hivi naishi hayo maisha sasa huwezi kuniambia Wema she is real. Mimi naishi hayo maisha by real sasa ndio maana kwake inakuwa changamoto, atafanya nini. Mimi ni changamoto kubwa sana kwa kila mtu ambaye yupo kwenye industry hii, maana sasa hivi unaweza ukaenda kwenye interview ukamfanyia msichana anayekuja interview akamtaja Gigy from nowhere pia. Mimi sifanyi kwaajili nashindana, nafanya kwa ajili yangu.”

Aliongeza kwa kusema kwamba walipokutana kwenye birthday ya Sallam, Wema Sepetu alinuna baada ya kumuona akikatika na Diamond Platnumz. Aliendelea kwa kusema

“Last time nimekutana naye hawezi kupiga stori na mimi tena, nimekutana naye kwenye birthday ya Sallam, nilicheza sana lakini nilikuwa ba bae Dangote. Alumina kweli na alikuwa ananiangalia vibaya lakini unajua ni mtu ambaye alishakuwa inspiration kwangu kwa hiyo siwezi kuonyesha action yoyote kwangu na kiukweli am the first person nilimwambia umependeza, wakati anaingia, am real. Ni kweli alivaa kizamani na umbo lake lilivyokubwa mashallah, alipendeza lakini nilivyopingia ndani tena sasa nilivyoitwa na Dangote kisa kuna Wema tena, niacheni kidogo siwezi kuvumilia. Sasa nikawa nacheza mimi na Dangote akawa ananiangalia mimi,”

About this writer:

Pauline Syombua

Content Developer IG: Kermbua