Gigy Money Amesema Hata Mo J Akiamua Kuoa Poa Tu

Video vixen a na msanii wa muziki wa Bongo fleva Gift Stanford ‘Gigy Money’ ameibuka na kuweka wazi kuwa hata leo ikitokea mzazi mwenzake anataka Kuoa kwake hana kipingamizi.

Hivi karibuni kupitia  ukurasa wake wa Instagram Mo J  aliposti picha akiwa na mwanamke mwingine huku akiwa amesindikiza maneno yaliyoashiria kuwepo kwa ndoa yao.

download latest music    

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la  Ijumaa, Gigy alisema kuwa kwa sasa hana tatizo lolote na mzazi mwenzie huyo, hata akiamua kuoa leo yeye hatojali chochote kwa sababu penzi lao liliisha muda mrefu hivyo wamebaki kama wazazi tu.

Hivi unajua mimi na Moj tulishaachana muda mrefu na kama mnavyoona ana mwanamke mwingine na mimi nina mwanaume wangu, kwa hiyo hata akiamua kuoa leo hii sitakuwa na pingamizi lolote ili mradi tu awe anatoa matunzo mazuri kwa mtoto wake”.

Gigy na Mo k walikuwa kwenye mahusiano kwa muda mrefu lakini Penzi Lao Lilivunjika Baada ya kukosekana uamifu Baina yao lakini walifanikiwa kuzaa Mtoto mmoja anayeitwa Mayra ambaye hivi sasa ana miezi sita.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.