Gigy Money Ampigia Magoti Mh Rais.

Msanii wa bongo fleva na ‘video vixen’ nchini, Gift Stanford maarufu kama Gigy Money ameiomba serikali ya Magufuli kuwapa msaada watanzania hususani wasanii, katika kulinda kazi zao sanaa ili kusudi waweze kutuliza akili zao sehemu moja nasio kutanga tanga na maisha.
Gigy Money ameeleza hayo alipokuwa anapiga stori na www.eatv.tv na kusema kwamba wasanii wapo tayari kubadilisha maisha yao ya mtandaoni na kufuata vile sheria za nchi zitakavyo, ila na wao wawaangalie namna ya kuwawezesha.
“Naiomba serikali ituangalie na sisi wasanii katika kazi zetu maana tunabanwa sana ndio maana utakuta wasichana wanaamua kujifyatua akili zao ili mradi apate pesa kwa njia yoyote, aweze kukizi mahitaji yake…..Tupo tayari kubadilika ila na wao tunaomba watusaidie baadhi ya vitu. Ninaamini sio mimi pekee yangu bali ni Tanzania nzima wanahitaji msaada, sema sisi tupo kwenye uoga sana, yaani watanzania wote ni waoga sana tena hususani wasanii pale inapokuja suala la kufungiwa kazi zao”, amesema Gigy Money.
Gigy Money ametoa kauli hiyo baada ya kupewa onyo na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza kuacha kutumia vibaya mitandao ya kijamii na endapo hatofanya hivyo basi watamchukulia sheria stahiki dhidi yake.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.