Gigy Money Amshauri Young Dee Kubaki Na Amber Lulu

Msanii wa kike ambae kwa sasa anatamba na kibao chake kipya cha ‘nampa papa’, Gift Stanford maarufu kama Gigy Money, mwisho ni mwa wiki iliyopita alijikuta akitoa povu zito kwa msanii mwenzie wa kiume anaejulikana kama Young dee kutokana na muenendo mbaya alionao katika mahusiano.kwa mujibu wa Gigy Money, Young Dee ni shemeji yake kutoka kwa Amber Lulu ambae pia ni msanii wa Bongo fleva lakini pia aliyekuwa na anaendelea kuwa moja ya ma-video queen wanaofanya   vizuri katika videos za wasanii mbalimbali wakubwa  nchini.

Gigy Money  alisikika akisema kuwa katika wanawake wote aliokuwa nao Young Dee ni msichana mmoja tu Amber Lulu ndie mwenye mapenzi ya kweli kwake sio hao wengine wanamchukulia kama kikatuni .Maneno hayo yalianza baada ya wasnii hao wote watuatu walipokutana nje ya jengo la EATV, wakitoka katika mahojiano ya kipindi cha Friday Nite Live ambapo , Amber Lulu aliona baadhi ya alama za kucha na vidole katika shigo ya Young Dee na kuanza kumshangaa na kumtuhumu kuwa itakuwa alikuwa katika ugomvi na mwanamke mwingine,

download latest music    

Kutokana na tukio ilo Gigy Money alipewa nafasi ya kuongea na kusema kuwa “Young Dee apunguze mitandao ya wanawake, maana inamchanganya wakati ukimwangalia umri wake ni mdogo sana,atulie tu na Amber Lulu maana katika wanawake wake wote mia  Amber Lulu ana mapenzi ya kweli kwake,wengine wote wanafata jina tu ilo la bongo bahati mbaya ,wanamuona kama kinyani wanamtakataka” alifunguka  Gigy Money ambae aliweka wazi pia kuwa kumbe wawili hao walikuwa katika mahusiano ya kimapenzi.

Amber Lulu na Young Dee walikuwa katika mahusiano ya kimapenzi kwa muda kidogo uliopoita huku wakikataa kuwa katika mahusiano hayo, ilifikia hatua mpaka Amber Lulu aliamua kuchora tattooo ya jina la  Young Dee mkononi lakini walipogombana Amber Lulu aliamua kufuta tattoo iyo, hivi karibuni pia kuna picha zilisambaa za amber lulu na Young Dee , picha ambazo ziliwafanya wawili hao kupelekana polisi .

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.