Gigy Money Amtolea Uvivu Irene Uwoya.

Msanii wa bongo fleva na ‘video vixen’ nchini, Gigy Money amefunguka na kumchana muigizaji wa filamu, Irene Uwoya kuwa umri wake umeshaisha wa kutengeneza ‘skendo’ za kuvaa na kupiga picha za nusu utupu na ndio maana anawasii watu wengine kuwa kama yeye.
Gigy ametoa kauli hiyo alipokuwa anazungumza na www.eatv.tv baada ya kupita takribani siku tano tokea mwanadada Irene Uwoya alipotoa kauli yake, ya kuwataka ma-star wenzake kuacha kutumia ‘skendo’ za kupiga picha nusu utupu kwa madai vitendo hivyo vinamchukiza hadi Mungu.
“Ana haki ya kuongea hivyo Irene, kwasababu ameshamaliza ujana wake wa kufanya vitu vya hivyo na anajua faida na hasara zake, ila sisi bado tutaendelea hadi pale tutakapoona imefikia tamati, ndio nasi tutaacha na kuwa kama yeye”, amesema Gigy.
Mbali na hilo, Gigy Money amesema mitandao ya kijamii imewasaidia kwa kiasi kikubwa kuwatambulisha katika jamii, jambo ambalo likapelekea na wao kuonyesha kipaji chao cha uimbaji walichokuwa nacho baadhi ya watu.
“Kinachoimba sio mavazi, mimi ninaamini kwenye kipaji zaidi kuliko kitu chochote. Lakini kama tungeanza kwenye muziki wasingetufahamu hadi hii leo na ndio maana kila mtu ana njia yake ya kujisogeza pahali fulani. Kwa hiyo waangalie u-serious wa mtu, vitu vingine ni ‘brand’ tu”, amesisitiza Gigy.

Gigy Money ni miongoni mwa wanadada walioweza kujipatia umaarufu mkubwa kwenye mitandao ya kijamii, kwa vituko vyake anavyovifanya kila kukicha bila ya kuhofia kitu chochote kilichopo mbele yake.

download latest music    

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.