Gigy Money Athibitisha Kuacha Kudanga Baada Ya Kuzaa

Msanii wa muziki wa Bongo fleva na video vixen maarufu Gift Stanford maarufu kama Gigy Money amefunguka na kudai Binti yake ndio alimuachisha yeye kudanga.

Gigy Money amefunguka na kuweka wazi kuwa kabla ya kuzaa alikuwa anatembea na wanaume ambao walikuwa wanamsaidia kipesa ambao kimjini Mjini wanaitwa madanga au sponsors.

download latest music    

Kwenye mahojiano aliyofanya na kituo cha habari cha BBC kupitia kipindi cha The She Word, Gigy Money ameweka wazi kuwa ameamua kuachana na tabia hizo kwa ajili ya binti yake Mayra ambaye ana Miezi kadhaa kwa sasa.

Nilikuwa na miaka kumi na saba nilikuwa najua nini nafanya na niliona ugumu aliokuwa anaupata mama yangu na mara nyingi tunafanya ili kupata hela lakini hatupendi hata kama ni njia rahisi ya kupata pesa, kilichonifanya nibadilike ni mwanangu sitaki aje kuwa kama mimi”.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.