Gigy Money Atoa Sababu za Kutaka Kuzaa na Mo-J

Mwanadada ambae ni mwanamuziki aliyejipatia umaarufu siku nyingi kutokana na kazi ya kuonekana katika video za wasanii mbalimbali na kujifunza na maswala ya muziki huko huko, Gigy Money amefunguka na kuelezea sababu ya kubeba mimba na kwa nini aliamua kuzaa na mwanaume aliyezaa nae kwa sababu watu wengi walikuwa wakihoji kilitojea nini mpaka Gigy Money aliamua kuzaa na kijana huyo ilhali kwa muda mrefu amekuwa akitaka kuwa katika mahusiano na wanaume wenye sifa za kuwa na hela nyingi.

zawadi kubwa nilikuwa natamani ilikuwa ni kuzaa na mo-j,ingawa watu wengi walikuwa hawajui ila ukweli ni kwamba mimi ndio nilikuwa natamani kupata mtoto siku zote.Sababu first he is cute lakini secondly ana mapenzi ya kweli kwa watoto kwa sababu unaweza kukuta kijana ni mzuri , handsome anavaa milegezo  lakini hapendi watoto yaani ukiwa na mimba tu na yeye anaanza kubadilika.

mo hii sio mimba ya kwanza kuwa nayo ya kwake ila hii ni mimba ya kwanza kuamua kuzaa na nilishawahi kubeba nyingine zikawa zinaharibika , zingine ninaharibu mwenyewe kwa sababu nilikuwa sina utayrai kwa kuwa sikuwa nina amini kuwa eti huyu ndo baba wa mwanangu.

Gigy money ambae kwa sasa anatamba na kibao kipya cha Mimina ni mjamzito wa mimba ya miezi saba, ambapo hivi karibuni aliwahi kulalamika kuwa mwanaume huyo aliembmbea mimba amekuwa akimpiga na kumtesa  pamoja na kwamba yuko katika hali ya ujauzito.

download latest music    

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.