Gigy Money Awekewa Masharti Makali Kwenye Nyumba Ya Kupanga

Video vixen maarufu na msanii wa Bongo fleva anayefanya vizuri na ngoma yake ya ‘Kiki ni Gigy’ Gift Stanford ‘Gigy Money’ amedaiwa kunyooshwa na mama mwenye Nyumba yake Baada ya kuwekewa masharti magumu.

Mtandao wa Global Publishers unaripoti kuwa Gigy alipewa masharti hayo magumu na mama huyo ambaye alikuwa anaijua historia ya msanii huyo kwani alikotokea aliwahi kugombana na mwenye nyumba mpaka kutaka kumshushia kipigo.

download latest music    

Kwenye mahojiano waliyofanya na mwanamama huyo aliyejitambulisha kwa jina la Mama Koku alifunguka:

Yaani Gigy alipoingia tu kwenye hii nyumba alipewa masharti makali kama vile kutovaa nguo za ajabu, kulewa, kuvuta bangi na kubadili wanaume hivyo akiwa anatoka kama amevaa nguo za nusu utupu anafunga kanga anaenda kuvua nje.

Sasa nilimwambia kwamba kama anataka kuishi vizuri na mimi hapa nyumbani kwangu sihitaji matusi na nilimpiga marufuku kuvaa vinguo vifupi hapa nyumbani kwa sababu nina watoto wadogo kwa hiyo sitaki waige tabia mbaya, nikamweleza kama anahitaji kuvaa nguo fupi awe anavaa akishatoka nje ya geti lakini siyo humu ndani.

Kuhusu kuvuta sigara na kutumia siwezi nikamzuia mtu kufanya kitu anachokipenda, pengine hiyo ndiyo furaha yake mimi nitajuaje, ila nashukuru Mungu kwa sababu naishi vizuri tu na huyu binti na ni mtafutaji sana, nampongeza kwa hilo“.

Gigy Money alipanga Nyumba hiyo ambayo ipo maeneo ya Kijitonyama mara Baada ya kumwagana baba wa Mtoto Wake Mo J na kuishia kutimuliwa kwake.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.