Gigy Money Bado Anamuwinda Diamond Platinumz

Mwanamuziki kutoka Tanzania asiyeishiwa na matukio kila kukicha Gigy Money  ameibuka na kuongelea jinsi gani anavyotamani kila siku kutoka kimapenzi na msanii mkubwa kutoka bongo Diamond Platinumz.Msanii huyo ambae kwa sasa anatamba na kibao chake cha papa ambacho kinafanya vizuri katika vyombo mbalimbali vya habari amefunguka bila kuwa na wasiwasi kuhusu hisia zake kwa msaanii huyo mkubwa kutoka Tanzania.

Akihojiwa na moja ya waandishi wa habari , aliulizwa kuhusu ndoto aliokuwa nayo muda mrefu ya kutaka kutoka kimapenzi na Diamond Platinumz, Gigy Money alisema kuwa yeye na Diamond wamekuwa wakiwindana kwa muda mrefu sana lakini yeye hana wasiwasi anaamini muda ukifika tu kila kitu kitakuwa sawa maana hajui kitu gani mwanamke mwenzie atakosea na yeye akapatia ili kuwa na Diamond lakini anaamini kabisa ipi siku hataweza kutoka na Diamond

download latest music    

iyo ndoto kama chemchem inachemka tu sijui lini mwenzangu,mimi na Diamond tunawindana, tukipishana baadhi ya sehemu tunaambiana tu wewe..wewe , lakini ninachoamini muda ukifika tu kila kitu kitakuwa sawa mambo mazuri hayataki haraka, na inawezekana hata tukadate, you never know wenzie watakosea wapi na wewe utapatia wapi, kila kitu kinawezekana” alifunguka Gigy Money

Gigy Money alishawahi kutangaza katika vyombo vya habari kuwa alikuwa na mahusiano na alikiba na kusema kuwa endapo wameacha lakini huwa wanakutana na kukumbushia mapenzi yake, hata hivyo alipoulizwa tena kuhusu hisia zake kwa msanii alikiba gigy money alisema kuwa kwa alikiba alishapita wala hana ya kurudi tena huko yeye saivi na diaond tu“kwa alikiba tulishapitaga huko, unajua ukipita sehemu kuja kurudi inakuwa  sijui unaonaje ..haaaa unarudiaa, saivi tunaenda mbele kwa mbele  kama ccm

Gigy Money ni moja wa wasichana wanaokwa wazi sana anapokuwa na mahusiano ya kimapenzi na wasanii, hivi karibuni amekuwa akiongelea sana kutamani kuwa na mahusiano na Diamond Platinumz huku akikana kurudiana na Rich Mavoko. Hata hivyo Gigy Money alikuwa katika mahusiamo na mtangazaji mwenzake wa radio moja wapo hapa nchini  na haijafahamika kama wameshaachana au la.

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.