Gigy Money , Lavalava Waamua Kuanika Penzi Lao Hadharani.

Haijapita hata wiki mbili tangu mwanadada Gigy Money alipowahi kuonekana akiwa katika mahaba mazito na mwanaume mmoja aliyesemekana kuwa akitokea Zanzibar ambapo kwa kipindi hicho Gigy Money alikuwepo na kusema kuwa mwanaume ndio anaetarajia kumuoa hivi karibuni huku akilalamikiwa kumuacha mtoto wake  mdogo akiwa na baba yake.

Wikiendhi hii , ilisambaa video nyingine ikimuonyesha mwanadada huyo akiwa na msanii kutoa WCB, Lavalava wakiwa katika starehe huku wawili hao wakiwa wanarekodi video fupi wakiwa katika mahaba huku wakishikana na kunyonyana miili yao.

download latest music    

Vitendo vilivyokuwa vikifanyika katika video hivyo havikuonekana kama ni vya kawaida kwa wasanii wanaofanya kazi pamoja au ukaribu wa kirafiki lakini urafiki wa kimahaba hivyo kuacha watu katikamshangao, lakini kubwa zaidi ni baada ya mwanadada huyo kuweka caption na kuandika “TUMEAMUA KUWEKA WAZI , TUMECHOKA KUJIFICHA ‘

Gigy money ambae hapo awali ilikuwa ikijulikana kuwa ana mtoto mdogo na kuwa katika mahusino na Mo jay , haijajulikana tena kama wawili hao wameachana au la mpaka sasa na hata hivyo katika ukurasa wa Mo jay wa instagrama amefuta kila kitu kinachomhusu Gigy Money.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.