H.Kaba kumaliza Beef Lake Na Diamond.

Msanii mkongwe alikuwa katika miondoka ya dansi H.Baba, ameamua kumaliza beef alilokuwa nalo na msanii mkubwa na anayefanya vizuri   kwa sasa bongo Diamond Platinumz kwa kuweka picha ya msanii huyo mkubwa akiwa na mzazi mwenzie Zari The Bossy hivi karibuni na kuandika maneno yenye kuonyesha kuwa hana chuki na wawili hao.

H.baba amesema kuwa amekuwa akivutiwa sana na mahusiano ya Diamond na Zari kwa muda mrefu na kwa sasa anawashauri waweze kuoana kwa kufunga ndoa na kama msanii mwenzie atatoa ngombe watano kwa ajili ya harusi hiyo.

download latest music    

H.baba ameongezea na kusema kuwa hawezi kuficha hisia zake kwa couple hiyo kwa sababu amekuwa akivutiwa nayo kila anapoiona ana amekataa kuwa kaa kwa kutaka kurudisha nyuma mahusiano hayo kwa sababu watu hao wanapendana na wamekuwa wakiendana sana.

Kinyama mnapendezana sana na mnaendnana sana , Mungu awasimamaie na kuwaongoza mfunge ndoa awe wako katika hesabu ya mwenyezo mungu,natoa ngombe watono kabisa wakubwa wa kisukuma waletwe Dar, huo nduo uwezo wangu  na hicho ndicho ntaajaliwa na Mwenyezi mungu.nakutakia maandalizi mema ya ndoa yako na hongera kwa kupendana……ninaheshimu mahusino yamtanzania mwenzangu#MIMINIMZALENDONANIMEKATAAKUWAKAA #Usinilazimishekwamanenoyakokuwakaa #Natudiatenanimekataakuwakaa.

Hii inakuja baada ya muda mrefu msanii h.baba kuwa katika beef zito na msanii diamond kutokana na kile kuwa msanii huyo alikuwa ni team alikiba kwa kuwa alikuwa akipost na kumsapoti alikiba huku akiweka vijembe vya kumkandia Diamond Platinumz.Hii inaongeza na kuwafariji mashabiki pale wasanii wanapokuwa wanapendana na kuungana ili kufanya kazi pamoja kwa sababu hii inaleta hamasa ya mashabiki kuzidi kuwapenda ,ashabiki.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.