Haitham aeleza faida ya kumshirikisha Wema Sepetu kwa wimbo wake – ‘Playboy’

Muimbaji Haitham alimshirikisha Wema Sepetu kwa wimbo wake mpya ‘Playboy’ ambayo alitoa siku mbili zilizopita.

Haitham amekiri kuwa amenufaika pakubwa na umaarufu wa Wema Sepetu. Akiongea na XXL ya Clouds FM, muimbaju huyo alisema kumshirikisha Wema kwa wimbo wake kumeongeza uzito wa jina lake.

download latest music    

“Toka nimetoa ngoma na Wema nimeona watu wamenipokea vizuri tena zaidi na zaidi lakini sio kwa sababu nimefanya na Wema pekee yake tu, kwa sababu ya muziki mzuri, watu pia wanasema muziki ni mzuri,” amesema Haitham.

Tazama wimbo wake hapo chini:

https://www.youtube.com/watch?v=OCHVKnItJE0

About this writer:

Martin Oduor

Ultimate keyboard ninja dedicated to bringing you the juiciest stories on blogosphere