Hakuna Mtu Aliyeumizwa na Msiba Wa Patrick Zaidi Yangu-Muna

Mwanamuziki wa nyimbo za Injili na mdau mkubwa wa Bongo fleva Rose Alphonce maarufu kama Muna Love amefunguka na kusema hakuna mtu aliyeumizwa na msiba wa mtoto Patrick Zaidi yake kama mama.

Muna amefunguka kutokana na maneno ambayo amekuwa akikumbana nayo Kwenye mitandao ya kijamii ambapo watu wamekuwa wakimponda kutokana na maamuzi yake ya kutumia Kifo Cha mwanaye kama ushuda kanisani.

download latest music    

Siku ya leo Muna alifanya mkutano na waandishi wa habari kwa ajili ya kutangaza Tamasha lake la Kidini litakalofanyika siku ya Jumamosi na aliweka wazi kuwa atatoa ushuhuda wake kuhusu Kifo Cha mtoto wake Patrick.

Kwenye mahojiano na vyombo vya habari, Muna alijibu tuhuma za kumtumia mtoto wake ambapo alifunguka:

Kwanza hakuna mtu anayeweza kusema ameumizwa na Kifo Cha Patrick zaidi ya mama mzazi na mimi tangu niingie Kwenye wokovu naamini hakuna mtu atakayeweza kuishi milele kila nafasi itaonja mauti lakini mimi natumia mwanangu ili kubasdilisha watu Ikiwa mimi mwanangu amenibadilisha nilikuwa mtu wa ajabu nilikuwa natukana na kufanya mambo mengi ya ajabu lakini niangalie leo hii nilivyobadilika”.

Mtoto wa Muna, Patrick alifariki dunia miezi michache iliyopita baada ya kuugua kwa muda mrefu.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.