Hakuna Mwanamke Wa Kunipindua Kwa Dogo Janja- Uwoya

Muigizaji wa Bongo movie mrembo Irene Uwoya amefunguka na kuweka wazi kuwa bado hajaona mwanamke ambaye anaweza kimpindua kwa mume wake staa wa Bongo fleva Abdul Chende ‘Dogo Janja’.

Uwoya ameweka wazi kuwa yeye ni mwanamke anayejiamini sana na anaamini kuwa mume wake anampenda na anajua kuwa hakuna mwanamke anayeweza kuingilia penzi lao.

download latest music    

Irene Uwoya amefunguka hayo Kwenye mahojiano na Global Publishers ambapo amesema alipoamua kuingia kwenye ndoa na mwanamuz­iki huyo alijua wazi ‘nyakun­yaku’ wapo, la­kini kikubwa anajiamini.

Mimi sio mwan­amke wa kufuatana na mume nyuma kwa sababu najiamiani kuliko na ninajua wazi hakuna ambaye anaweza kunin­yakulia mume wan­gu. Najiamini kila idara mimi sina wasiwasi wowote”.

Uwoya amesisitiza kuwa hata mume wake aende wapi na aone mwanamke gani hawezi kumuacha yeye maaana anajiamini na anaamini kuwa amekamilika idara zote.

Uwoya na Dogo Janja walioana mwaka jana ambapo wiki iliyopita walifikisha miezi Tisa katika ndoa pamoja.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.