Hamisa Alinitolea Povu Kisa Kumshauri Diamond Anunue Kondomu- Idris Sultan

Muigizaji wa bongo movie na mchekeshaji maarufy Idris Sultan amefunguka na kukiri kuwa moja kati ya matukio anayokumbuka sana kwa mwaka 2017 ni pale ambapi Hamisa alimtolea povu zito Kisa kumshauri Diamond anunue kondomu.

Idris ni moja kati ya comedians aliyekiki sana kwa mwaka uliopita na amekiri kuwa moja kati ya matukio yaliyomuingiza matatani kwa mwaka uliopita ni pale alipomtania Diamond atumie kondomu kwenye birthday yake ili kuepusha kuwapa mimba wanawake wengine anaochepuka nao maneno yaliyomkera Hamisa na kusababisha kumtolea povu zito.

download latest music    

Alipokuwa anafanya interview na Millard Ayo TV Idris Sultan alifunguka yafuatayo kuhusiana na sakata hilo kati yake na mzazi mwenza wa msanii Diamond Platnumz:

Kilichotokea ni kuwa ilikuwa birthday ya Diamond so kiutani kabisa nikamshauri Mondi anunue Kondomu nikampa shilingi mia tano kusema kweli ilikiki sana mtandaoni lakini ilibidi nifute kwa sababu Hamisa alinimind sana kwa kitu kile na mimi niliona kuwa ilimgusa sana kimtindo alafu ukiangalia yule ni mama ingawaje utani sio mbaya lakini kwa lile nilifuta ile posti lakini sikuishia hapo nilimuomba na msamaha na ninaamini alinisamehe na tukayamaliza”.

Idris amekiri kuwa mwaka 2017 ulikuwa mzuri  kwake Lakini zaidi amesisitiza kuwa anategemea kuwa na mwaka mzuri zaidi kwa mwaka 2018 kwani anategemea kucheza filamu yaje itakayo fanyika nchini Marekani Hollywood  na mambo mengine mengi aliyoandaa maalumu kwa mashabiki zake.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.