Hamisa Amtolea Povu Zito Idris Sultan

Mchekeshaji maarufu Idris Sultan amejikuta katika wakati mgumu baada ya Hamisa Mobetto  kumwagia povu zito. Hii ilitokea pale ambapo Idris alimuandikia Diamond ujumbe wa birthday na kumtaja Hamisa na mtoto wake.

Idris alimuandikia Diamond ujumbe huu;

download latest music    

“Dear Diamond nimekaa nikawaza sana ila nimemaliza na jibu nimepata Kama kaka au mshikaji wako nimeona kuna vituo vingi Sana vya watoto wasio ma uwezo wa kujisomesha na hata chakula hakitoshi, nimeona kuna vijana wengi hawana ajira, nimeona kuna wengi hawajui kesho wataamkaje. Kwa sasa wewe unaweza kuwasaidia sana  utakua unajiuliza hii mia 500 ya nini ila nimegundua nikikupa hii mia 500 ntakuwa nimeokoa maisha ya watu wengi Sana. Hii mia 500 nunua condom ili hizo elfu 70 tuwe tunatoa misaada name Rav 4 zitapeleka mchele orphanage Happy birthday brother”.

Ujumbe huo ulionekana kumkera Hamisa na kupelekea kumjibu Idris kupitia ukurasa wake Wa Instagram aliandika;

“Okay your just too much Iddy Honestly speaking…..Nadhani we ndo mtu pekee uliokazania elfu 70 na Rav 4 kuliko hata huyo aliyetoa mwenyewe…..Mtoto anapangwa na Mwenyezi Mungu kumbuka wakati hiyo gari inatolewa haikutolewa wakati nina mimba or kisa ya mimba ilitolewa kwa mapenzi na iyo elfu 70 ilitolewa kwajili ya mapenzi coz mtoto alikuwa hajazaliwa yet, Kindly stop using this to hurt me or my son….Kusaidia watoto wasio na uwezo ni jambo jema Sana and am sure you can tell him/ask him afanye hivyo without kutumia ishu yangu au mtoto wangu kama source”.

Baada ya kuona hali imekuwa hivyo Idris kwa kupitia ukurasa wake wa instagram alimuomba msamaha  Hamisa na wanawake wote aliowakosea kupitia ujumbe wake kwenda kwa Diamond.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.