Hamisa Atupilia Mbali Kesi Ya Madai Kwa Diamond.

Baada ya kesi ya mwanadada mrembo aliyefanya vizuri katika video mbalimbali nchini za wasanii  wengi Hamisa Mobeto kuhusu madai ya malezi ya mtoto wake kwa kiume kwa baba wa mtoto huyo Diamond Platinumz kuonekana kuwa ilikosewa kufunguliwa na kutakiwa kurudiwa kufunguliwa upya, inasemekana kuwa kesi hiyo imefutwa kabisa baada ya mwanadada huyo kusema kuwa ameona ni bora atupilie mbali kesi hiyo na kuamua kupatana na baba wa mtoto.

Wawili hao ambao wamebahatika kupata mtoto mmoja kwa muda mrefu walikuwa wakionekana hawako vizuri katika mitandao ya kijamii na kuwa wanajibizana lakini hivi karibuni mwanadada huyo amesema kuwa haikuwa na maana ya kuendelea kupigana na kesi hiyo mahakamani kwa sababu wameshakubaliana na mzazi mwenzie.

download latest music    

Kampuni ya GPL walipomtafuta hamisa kuthibitisha kauli hiyo alisema kuwa ni kweli kesi hiyo imefutwa na wapo vizuri na baba wa mtoto wake.

Kwanza sitaki kuzungumzia hizo habari kabisa,lakini ujue tu kuwa hakuna kesi yoyote inayoendelea na tuko vizuri na baba wa mtoto.

Hamisa alifungua kesi hiyo kumshitaki Diamond ambae alikuwa akisema katika media kuwa alikuwa akimpa Hamisa ela ya matunzo ya mtoto ilhali kwa anavyosema yeye kuwa sio kweli, hivyo Hamisa alifungua kesi hiyo ili kuwa anapewa haki ya mtoto wake kupitia sheria za mahakama.hata hivyo watu wengi waliamua kuwashauri wawili hao kuweza kukaa na kutafakari swala la kwenda mahakani ni kubwa kuliko wakikaa pamoja na kuongea kama familia.

Swali kubwa kwa mashabiki linakuwa je kama wawili hao wamepata au kukubaliana kuhusu malezi ya mtoto , inakuwaje kwa mzazi mwenzie na Diamond, yaani Zari ambae alikuwa katika vita kubwa na Hamisa katika kumtetea mumewe.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.