Hamisa Mobeto Akumbuka Wema wa Mange Kimambi.

Ikiwa  siku ya tarehe 4 March ni siku ya kumbukumbu ya mwanaharakati wa kimitandao Mange Kimambi , amepokea salamu nyingi sana kutoka kwa watu mbalimbali huku yeye mwenyewe akisema kuwa hata baadhi ya upinzani wake waliweza kumtakia kheri ya siku hiyo ya kuzaliwa kwake.

Moja ya watu maarufu wanao-trend sana katika mitandao kwa sasa Hamisa Mobeto pia alikuwa ni mmoja walimtakia dada huyo kheri katika siku yake ya kuzaliwa lakini hii haitoshi kuelezea hisia zake hadi pale alipoamua kutoa shukrani zake za moyoni kuhusu mwanaharakati huyo na kwa jinsi alivyosimama nae kipindi cha matatioz yake.

download latest music    

Hamisa alimpongeza mwanadada huyo kwa siku hiyo lakini pia alimwambia kuwa anamshukuru sana kwai kipindi anapata matatizo ya kugombana na Zari na Diamond kila siki yeye hakuwahi kuonyesha kuchukia zaidi ya kumsapoti na kumtia moyo na hata wakati mwingine kutoa ushahidi wa ukweli kwa watu.

Happy birthday da mange @mangekimambi …wakati wengi waliniacha ulisimama nami  na pia wakati wngi walivyokuwa  hawaniamin you did..napenda kusema ahsante sana.

Mwenyezi Mungu ndo pekee anajua jinsi gani ulivyonipa nguvu  na ujasiri my dada.May Allah guide and protect you mama… na asante sana.-Aliandika Hamisa Mobeto katika ukurasa wake wa instagram.

Tukumbuke kuwa shukrani yake kwa Mange inakuja pale ambapo Hamisa alipokuwa akigombana sana na Diamond pamoja na zari kuhusu nani ni mmiliki halali wa mimba aliyokuwa nayo Hamisa, na hata mtoto alipozaliwa mange kimambi alishawahi kusema wazi kuwa mtoto ni wa Diamond Platinumz, siku zote ya vita kati aya pande hizi mbili Mange kimambi alikuwa akiandika posti za kumtia moyo Hamisa na ilipobidi kutoa ushahidi kwa kukandamizwa kwake Mange Kimambi aliweka ushahidi hadharani.

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.