Hamisa Mobetto Amefunguka Haya Baada ya Kusuluhishwa na Diamond

Msanii na mwanamitindo maarufu Hamisa Mobetto amefunguka baada ya kusuluhishwa na mzazi mwenzake supastaa wa Bongo fleva Diamond Platnumz mahakamani siku ya jana.

Baada ya vita ya mitandaoni kuendelea kwa miezi kadhaa tangu mtoto wao azaliwe pande zote za familia zao zimekuwa zikionyesha kukwaruzana huku Diamond na Hamisa kuonyesha kutoelewana kuhusu mambo yao mbali mbali.

download latest music    

Siku ya jana Hamisa na Diamond wote walifika mahakama ya hakimu mkazi Kisutu kwenye mahakama ya watoto ambapo waliitwa ili kumalizia kesi hiyo Hamisa na Diamond wote waliongelea kuhusu kusuluhishwa na kupatana kwao.

Kwenye mahojiano na Millard Ayo Tv, Hamisa alifunguka yafuatayo;

Leo sana sana kulikuwa kuna kama suluhisho na mwisho wa kesi na kila kitu that’s why ilibidi wazazi wote wawili ilibidi tuwepo na tuonekane tupo pale na kuyamaliza, ilikuwa ni kuhusu kumuhudumia mtoto na vitu vingine kwaiyo tumeshakubaliana kuwa atamhudumia mtoto wake na hivyo yaani.

Kama ilivyokuwa kwa watu wengi kila mtu alikuwa anataka kujua endapo Hamisa kapata kiasi alichokuwa anataka kwa mwezi milioni 10, Hamisa alisema haya:

Hayo ni mambo ya kifamilia siwezi kusema ila hata kama ikiwa milioni mia ni sawa tu kama mzazi ana uwezo sawa tu haina tatizo kwa sababu mwisho wa siku inategemeana na uwezo wa mzazi ila kiasi cha pesa tulichokubaliana siwezi kukisema kwani sitakiwi kukitaja kwa sababu ni mambo ya kifamilia zaidi.

Unajua kwenye familia kuna pande mbili upande wa mama na upande wa baba hawa watu kwa kujua au kutokujua hawakuwepo pale wakati mtoto anatengenezwa au hawajui njia gani aliyotengenezwa  but kila mtu anakuwa na la kusema mwishowe inasababisha makelele ila nashukuru yameisha hakuna mzazi anayependa mtoto wake kusemwa vibaya”.

Hamisa amehitimisha kwa kusema hana ugomvi na Diamond na ana imani huu utakuwa mwanzo mzuri wa kuendelea kumlea mtoto wao lakini pia amesisitiza kuwa hana mpango wa kuolewa kwa sasa kwani haamini masuala ya ndoa na ndio maana amezaa nje ya ndoa.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.