Hamisa na Zari Ndani Ya Uganda Siku Moja.

Imepita muda mrefu zile chokochoko za wanawake wawili Zari The Bossy pamoja na Hamisa Mobeto  zimetulia katika mtandao na kukawa na matumaini kuwa wasichana hao wawili ugomvi wao utakuwa umeisha , lakini kumbe sio kama vile watu wanavyofikiria kwa sababu inawzekana hichi kinachokuja sasa hivi kikawa ni  kikubwa zaidi.

Ni muda mrefu tangu Zari The Bossy Lady atangaze kuwa atakuwa na party yake inayifanyika uganda kila mwishoni  mwa mwaka inayojulikana kama zari all white party, na kweli party hiyo imeshaanza kuwa na maaandalizi yake nchini Uganda, lakini kitu cha kushangaza na kujiuliza ni kwamba Hamisa pua ametangaza kufanya party yake nchi Uganda siku moja na ile ambayo Zari anategemea kufanya party.

download latest music    

Tarehe 21 December, Zari atafanya party nchi Uganda na siku hiyo hiyo Hamisa Mobeto mrembo kutoka Tanzania anategemea kufanua party yake nchini humo, hii ina maana gani , je ni kweli kuwa sasa Hamisa ameamua kushindana na Zari mpaka kwenye maswala kama hayo, je anataka kumuaribia soko au waandaaji wa tamsha hilo kutoka Uganda wameona hiyo ndio njia sahihi ya kumzima Zari.

Zari na Hamisa Mobeto waliingia katika bifu zito baada ya hamisa mobeto kuingia katika mahusiano ya kimapenzi na mzazi mwenzie na Zari ,Diamond Platinumz, ambapo wawili ho walifanikiwa kuzaa mtoto mmoja wa kiume.

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.