Harmo Rapa Adai Anajutia Kuwa Mtu wa Kiki

Msanii wa Bongo fleva Harmorapa ambaye pia ni maarufu sana Instagram kwa kupenda kutafuta kiki ameibuka na kudai anajutia sana kutafuta kiki kutokana na kinachoendelea hivi sasa.

Harmo Rapa amekuwa Kwenye headlines kwa sababu yeye na Mrembo anayeitwa Khadijah wamekuwa wakijibizana ambapo msichana huyo anadai yeye na Harmorapa ni wapenzi lakini mwenyewe anakataa na kudai msichana huyo anatafuta tu kiki na hawana Mahusiano.

download latest music    

Sakata hilo lilitokea siku ya Ijumaa iliyopita ambapo kwenye studio za EATV katika kipindi cha Friday Night Live, Harmorapa na Khadijah waliingia kwenye ugomvi baada ya Khadijah kudai anaweza kuthibitisha kuwa ana Mahusiano ya Kimapenzi na Harmorapa na kudai ana kovu Kwenye sehemu za siri.

Baada ya kuambiwa hivyo basi Harmorapa aliondoka Kwenye studio hizo kwa hasira na kufanya mahojiano na Kipindi cha Enews cha EATV ambapo amedai kwa sasa anajutia kiki yake na Khadijah.

Harmorapa amekiri kuwa yeye kutangaza kuwa Khadija ni mpenzi wake ilikuwa ni kiki tu lakini hampendi msichana huyo imemkera Khadija kwani amekuja juu na kumtaka Harmorapa amlipe pesa zake alizompa kwa ajili ya kiki hiyo jambo lililomfanya Harmorapa Akiri anaachana na kiki.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.