Mabishoo wamtupia chupa Harmorapa akitumbuiza Maisha Basement

Image: Harmorapa

Harmo rappa alinusurika kifo usiku wa Jumapili 02 April 2017, baada ya kupigwa chupa na shabiki mmoja akiwa stejini. Msanii huyo alikuwa na show ya ‘USIKU WA KOMELA’ na kama kawaida mashabiki walijitokoza kwa wingi kumuona star huyu akiwatumbuiza.

 

download latest music    
Harmo rappa atupiwa chupa stejini
Harmo rappa atupiwa chupa stejini (photo credits)

Hata hivyo, Harmo rapper alipopanda jukuani kuperform wimbo wake mpya ‘Kiboko ya mabisho’ alishtukia akirushiwa chupa iliyokuwa na bia na mmoja ya mashabiki aliyekuwa ukumbuni mwa mashabiki wenzake.

Kulingana na ripoti shabiki huyo alitupa chupa hiyo baada ya Harmo rappa kuimba mstari mfupi wa wimbo wake, tulikuwa WASAFI kabla ya WCB, maneno yao machafu hayaniharibii CV…. ulio mkasirisha shabiki huyu mkubwa wa wasafi.

Shabiki aliyemtupia Harmo rappa chupa stejini
Shabiki aliyemtupia Harmo rappa chupa stejini

Hata hivyo chupa hiyo ya bia haikumfikia Harmo rappa kwani alikwepa na kuitoraka. Baada ya tukio hilo, klabu ya Maisha Basement wasiwasi lakini bouncers waliweza kumtoa rappa huyu stejini kabla ya kumtafuta kijana aliyesababisha fujo hizo.

Baada ya muda jamaa huyo alipatikana na bouncers waliomhoji kujua kilichomsababisha kufanya kitu kama hicho. kuwa ameshachakazwa na wananchi wenye hasira kali. Kulingana na alichosema, inaonekana huyo hakuwa shabiki wa Harmo rapper. Hata hivyo alikamtwa na kupelekwa polisi na sasa hivi anangoja kupelekwa kotini.

 

About this writer:

Pauline Syombua

Content Developer IG: Kermbua