Harmonize Afunguka Baada Ya Kumwagana na Sarah

Staa wa muziki kutoka WCB Harmonize amefunguka kwa mara ya kwanza tangu sakata litokee wikiendi iliyopita na kusababisha yeye na mpenzi wake Sarah kutofautiana.

Harmonize na Sarah walikamata headlines mwishoni mwa wiki hii baada ya wawili hao kurushiana maneno Kwenye mitandao ya kijamii na hata matusi yaliyopelekea kumwagana baadae.

download latest music    

Harmonize anafunguka kuhusu sakata hilo na kuweka wazi kilichokuwa kinatokea pale ni wivu wa kimapenzi ambao Sarah anao juu yake hasa pale alipomuona akiwa na wadau wa muziki wa kike.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Wasafi Tv, Harmonize anafunguka kuhusu sakata hilo lililotokea kati yake na Mpenzi wake Sarah:

Unapoamua kuwa na mtu unatakiwa ujue huyo mtu ni wa aina gani, anafanya kazi gani, ukishajua hivyo unakuwa ni rahisi zaidi ku-deal naye.

Nakutana na watangazaji, wasanii inatakiwa ni badilishane nao mawazo, sasa ukiwa unaendekeza kila saa masuala ya kimahusiano inakuwa unanirudisha nyuma kwa namna moja au nyingine”.

Harmonize ameweka wazi kuwa sakata  hilo lilianza baada ya Sarah kujaribu kumpigia kwa muda mrefu na yeye kutokana na kuwa bize na kazi alishindwa kupokea simu na hivyo kusababisha kukosa maelewano.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.