Harmonize Afungukia Ishu Ya Kuondoka Katika Lebo Ya Wasafi

Mwanamuziki wa bongo fleva anayefanya vizuri na nyimbo sake mbili hivi sasa ‘shulala’ na ‘nshachoka’ kutoka katika lebo ya Wasafi classic amefunguka kuhusu ishi ya yeye kuihama lebo hiyo.

Harmonize aliamua kulizungumzia jambo hilo baada ya kudai kuwa watu wengi hasa mashabiki zake wamekuwa wakimuuliza mara kwa mara kama ipo siku ana mpango wa kuhama lebo hiyo ambayo ndio chanzo cha mafanikio yake kwani ndiyo iliyomtambulisha kwenye muziki miaka michache iliyopita ijapokuwa safari yake ya muziki ilianzia mbali kwani ni miaka michache tu Harmonize alikataliwa kwenye shindano la kutafuta vipaji la Bongo star search.

download latest music    

Kwenye mahojiano na Times FM kwenye kipindi cha The playlist Harmonize alifunguka:

Kuhusu suala la mimi kuhama WCB naomba niseme hapana kwa kweli kwani unapokuwa unamzungumzia Harmonize unakuwa unaizungumzia Wasafi classic baby na unapoizungumzia WCB unamzungumzia Harmonize pia yaani hiyo kama baba kama mama na pia isitoshe naikubali familia nzima ya WCB kwani kila mmoja wetu ana kipaji hakuna aliyekuja pale kwa Bahati mbaya yaani kikubwa wote tunatofautiana”.

Ni vizuri kwa wasanii kuwa na uangalizi yaani management kwani sahuvi muziki umekuwa biashara kama biashara nyingine kwaiyo msanii yoyote anahitaji timu nyuma yake ili kufanikisha malengo take binafsi.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.