Harmonize Akana Tetesi Za Kumchumbia Sarah

Staa wa muziki wa Bongo fleva kutoka katika label matata WCB Harmonize ambaye kwa sasa anafanya vyema kabisa na ngoma yake ya ‘Kwangwaru’ amefunguka na kukataa tetesi zinazodai kuwa amemvisha Pete mpenzi wake Sarah.

Tetesi za Harmonize kumvusha pete ya uchumba mpenzi wake Sarah zilianza kusambaa wiki chache zilizopita baada ya kuposti picha Kwenye mitandao ya kijamii zikiwaonyesha Harmonize akimvisha pete ya thamani Sarah.

download latest music    

Tukio hilo la kuvalishana pete lilionekana kwenye mitandao ya kijamii siku chache baada ya wawili hao kugombana na kurushiana maneno kwenye Instagram baada ya Tetesi za Harmonize kuchepuka.

Kwenye mahojiano aliyofanya alipokuwa nchini Kenya kwa ajili ya shoo yake Harmonize aliwaambia Pulse Live kuwa hajamvalisha pete ya uchumba Sarah kama Tetesi ila wapo mbioni kufanya hivyo:

Sijamvisha Pete mchumba wangu,… na Ndoa bado unajua siku zote ndoa ni mipango na ikifika wakati wa engagement nitawatangazia”.

Mwezi uliopita Harmonize alikumbwa na tetesi za kuchepuka na wasichana kadhaa ikiwemo msanii wa nyimbo za Injili kutoka Kenya na mtangazaji kutoka Nigeria lakini pia Ex wake Jacqueline Wolper.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.