Harmonize Aliniumiza Alipoweka Jina la Mume Wangu:Shamsa

Mwanadada Shamsa Ford kutoka bongo movies amefunguka kwa mara ya kwanza akiongea na waandishi wa habari na kusema kuwa kitendo cha Harmonize kuweka jina la mume wake katika list ya wanaume aliwahi kutembea nao Jackiline Wolper ilimuumiza sana kwa sababu ni mtu anaempenda.

Shamsa Ford amesema hayo siku ya uzinduzi wa filamu ya mama ya Aunty Ezekiel wikiendi iliyopita na kusema kuwa hata kama asingekuwa mke wake lakini swala  hilo lililmuumiza sana kwa sababu ni mambo yaliyopita tayari.

download latest music    

Ni lazima uumie kama binadamu na kwa sababu ni mtu unaempenda,lazima uumie tu na sio kwa mume tu hata kwa mtu ambae ni part ya maisha yako utaumia.

Siku chache zilizopita kulitokea mtafaruko kati ya harmonize  na aliyewahi kuwa mpenzi wake jackline wolper na ambapo harmonize kwa kutaka kumuhaibisha jackline aliamua kutoa idadi na majina ya wanaume aliwahi kutoka nao jacky kimapenzi ambapo kati ya majina hayo pia kulikuwepo jina la Chid Mapenzi ambae ni mume wa ndoa wa Shamsa Ford.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.