Harmonize Amefunguka Kuhusu Bifu Lake na Idris Sultan

Msanii kutoka label ya WCB, anayefanya vizuri hivi sasa na ngoma yake ya ‘shulala’ Harmonize amefunguka na kudai hana bifu lolote na mchekeshaji Idris Sultan.

Habari za wawili hawa kuwa na bifu zilienea miezi michache iliyopita mara baada ya Idris kuandika mtandaoni kuwa Harmorapa alikuwa anafanya vizuri kuliko Harmonize na hivyo ni bora Harmonize astaafu kufanya mziki maneno hayo yalimkera sana Harmonize ambaye alimuita Idris shoga mtandaoni. Tangu siku ile inadaiwa wawili hawa hawaivi kabisa katika chungu kimoja.

download latest music    

Kwenye mahojiano aliyoyafanya na Times Fm Harmonize amedai kuwa hana bifu lolote na Idris na anashangazwa maneno hayo yametoka wapi.

Sina bifu na Idris na sijawahi kuonana naye, I am telling you ni stories tu naona watu wanatengeneza kila siku alafu kingine mi ni mtu wa kusamehe sana haya mti akiwa amenikosea kabisa  naamini ni binadamu tu kwani hata might naamini huwa kuna watu nawakoseaga”.

Harmonize ambaye anazidi kufanya vizuri na wimbo wake wa shulala umekuwa ukishika namba moja katika stesheni mbalimbali za redio na hata kwenye mtandao wa video YouTube bado unaongoza.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.